• Mwanzo
  • Kuhusu
  • Mbio
  • Habari na Picha
  • Matokeo
  • Vifurushi
  • Wadhamini
  • Wasiliana Nasi

ENG

ENG

ENG

  • Mwanzo
  • Kuhusu
  • Mbio
  • Habari na Picha
  • Matokeo
  • Wadhamini
  • Wasiliana Nasi

ENG

ENG

ENG

 

Tulipotoka….

Kwa miaka zaidi ya 25 Benki ya CRDB imeshiriki katika kutoa mchango kwa jamii inayoizunguka kupitia utoaji wa huduma za fedha sambamba na kurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii. Katika kipindi chote hiko, Benki ya CRDB imekua ikiamini katika nguvu ya ushirikiano ili kuleta matokeo chanya.

CRDB Bank Marathon ni mbio za hisani zilizoanzishwa na Benki ya CRDB mnamo mwaka 2020 zikiwa na lengo la kuunganisha mtu mmoja mmoja, vikundi na taasisi mbali katika kushiriki mbio na kujenga afya za miili yao huku wakitatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii.

Ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika nchini Tanzania katika jiji la Dar es Salaam, CRDB Bank Marathon iliweza kuteka hisia za watu wengi kupitia kauli mbiu ya “Kasi Isambazayo Tabasamu”.

Msimu wa kwanza wa CRDB Bank Marathon ulilenga kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia upasuaji wa watoto 100 wenye matatizo ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).  Zaidi ya wakimbiaji 4,000 kutoka ndani na nje ya nchi wakishiriki mbio hizo kwa mara ya kwanza ambapo kiasi cha Shilingi Milioni 200 ziliweza kupatikana na kufanya mbio hizo za kwanza za CRDB Bank Marathon kuweza kufikia lengo.

 

 

 

 

CRDB Bank Marathon inahusisha mbio za 65km kwa waendesha baiskeli, 42km, 21km, 10Km na 5km kwa wakimbiaji kwa miguu ambapo wote hupimwa uwezo wao kwa teknolojia ya kisasa inayowezesha kujua muda waliotumia kukimbia. Hivi sasa, CRDB Bank Marathon si jina geni kwa wanariadha huku zikitajwa kuwa moja kati ya mbio bora zaidi kuwahi kutokea nchini Tanzania na Afrika Mashriki pamoja na kuanzishwa hivi karibuni.

Pamoja na kutambulika kama tukio la kimichezo na kijamii lakini pia CRDB Bank Marathon ni tukio la burudani lenye kukutanisha familia, marafiki na washirika wa kibiashara pamoja baada ya mbio ambapo watu hufurahi pamoja kwa burudani mbalimbali ikiwemo muziki, nyama choma na michezo ya watoto. Hakika CRDB Bank Marathon ni tunda jema lilichipuka katika ardhi ya Tanzania na kuleta matumaini chanya kwa wanamichezo na jamii nzima ya Tanzania kwa kutoa fursa za kimichezo, kijamii na kiuchumi.

 

 

Safari Yetu

Mwaka 2021 umeanza kwa tabasamu kubwa kwa wapenzi na washiriki wa CRDB Bank Marathon ambapo imeweza kuthibitishwa kufikia viwango vya kimataifa na Chama cha Mbio za Kimataifa (AIMS) kwa kushirikiana na Shirikisho la Kimataifa la Riadha (World Athletics). Ni wakati sasa ambapo CRDB Bank Marathon inauleta ulimwengu pamoja na kusambaza tabasamu kwa jamii yetu.