ENG

ENG

ENG

ENG

ENG

ENG

Kuhusu CRDB Bank Marathon

CRDB Bank Marathon ni mbio za kimataifa zinazotoa fursa kwa jamii, wateja, taasisi washirika watanzaniana washirika duniani kote kushirikiana na Benki ya CRDB kutoa mchango katika jamii katika nyanja za elimu, afya na mazingira.CRDB Bank Marathon ni fursa kwa jamii na dunia nzima kusaidia kuboresha jamii yetu na kusambaza tabasamu kwa watu wenye uhitaji. Karibu tusambaze tabasamu! 

Ujumbe kutoka Menejimenti

"Kupitia sera yetu ya kusaidia jamii tumekuwa tukishiriki katika kuboresha maisha ya jamii yetu na kuleta maendeleo katika nyanja za elimu, afya na mazingira. CRDB Bank Marathon inatupa fursa ya kushirikiana na wateja, wadau wetu wa biashara na Watanzania wote katika kutatua zaidi changamoto zinazoikabili jamii yetu".

Mbio za mwaka huu za CRDB Bank Marathon zinatarajiwa kukusanya takriban bilioni moja za kitanzania ambazo  zitakwenda  kusaidia uchangiaji wa gharama za upasuaji kwa watoto wenye matatizo ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya  Jakaya Kikwete (JKCI) kwani uhitaji bado ni mkubwa na pia kampeni ya CCBRT ya kuboresha matokeo ya afya ya uzazi kwa wanawake wenye ujauzito hatarishi (High Risk Pregnancy). Lengo letu na  JKCI ni kusaidia angalau watoto 100 kutoka katika familia zisizojiweza kufanyiwa upasuaji wa moyo. Kwa upande wa  CCBRT, lengo ni kuwasaidia angalau wanawake 100 wenye ujauzito hatarishi.

Abdulmajid Mussa Nsekela

Tully Esther Mwambapa

Mkurugenzi wa Mawasiliano.

Mkurugenzi Mtendaji.